MKOA WA SONGWE NINAOUTAKA

Usisahau kufika Ndolezi kuona na kugusa KIMONDO

15/ JULY 2019 MKOA WA SONGWE ULIANZISHWA JANUARI 29/2016, SASA UFUNGUKE

TUTAZAME MIUNDOMBINU:- Mkoa wa Songwe ulivyokaa na miji mikuu yake Mlowo, Vwawa, na Tunduma, na Ofisi ilipo. Ofisi ya mkuu wa mkoa siyo vema ikategemea Lango moja. Inahitaji miundombinu ya barabara zifuatazo, kiwango cha Lami. Barabara ya kutoka Vwawa, kupitia Muzunguko, Ndolezi (Kimondo) mpaka Mahenje. Barabara ya kutoka Nselewa (ofisi ya mkoa) mpaka Mzunguko. Tukiboresha hizo ofisi ya mkoa itakuwa imefunguka. Lakini pia tusisahau kuweka hifadhi ya barabara ya pili kutoka Mulowo mpaka Tunduma kabla watu hawajajenga sambamba na barabara kuu ya Tunduma. Hili litaepusha bomoa bomoa zisizo za msingi kwa jiji tarajiwa la Songwe na kulipanga jiji mapema kabla halijashona. Kuwepo mkakati wa kujengwa ukumbi wenye hadhi ya kimataifa sambamba na kitovu cha biashara za wasambazaji wakubwa kama tunavyoiona Kariakoo leo Dar.es Saraam. tunaweza kuibuka na kitu cha ziada, ukizingatia Songwe ni mpakani, hii itaongeza kasi ya utalii na malipo ya kodi pia yataongezeka. Wadau toeni mawazo ya kitaalam hapo mwisho wa ukurasa huu. Asante sana.

31/03/2024 Maendeleo huletwa na nguvu ya pamoja kwa juhudi na maarifa. Sasa tunaiona Barabara ya kutoka Vwawa kupitia Mzunguko, kuelekea Ndolezi (kwenye KIMONDO) ipo hatua za mwisho kwa kiwango cha lami.

Barabara inayoonekana hapo ni Mzunguko kona ya kutoka Nselewa maarufu MKOAN au Kibao cha Mahakama. sasa ni wakati muafaka viongozi wetu kuitupia jicho hii barabara kama sehemu ya kuendelea kuyafungua makao makuu ya mkoa wa Songwe.

10/03/2023:- SHULE ZETU SASA ZINAHITAJI TEHAMA ILIYO JITOSHELEZA.

Jukumu hili lichukuliwe na wananchi kwenye shule zao ili kuboresha huduma ziendane na Dunia ilpofika. kazi nyingi sasa zinafanyika kwenye kompyuta. lakini shule zetu hazijawezeshwa kwa hilo.

Nini kifanyike?

Kwanza Kuna baadhi ya shule za sekondari zinapata wadhamini wanaoweza kusambaza TEHAMA hawa wapewe mashariti ya kiwango cha vifaa vya kupeleka. Mfano shule inapewa kompyuta na Printer. computer sina shida nayo, shida printer. Shule ni taasisi unapoipa printer ya matumizi ya nyumbani ikatumike kwenye taasisi ni kuwapa mzigo walimu na kushinda kwa mafundi printer bila sababu. Hizo printer ziwe na mashariti kuwa ukiamua kufanya hivyo basi fuata vigezo peleka mashine ya kiwango cha taasisi.

Pili viongozi wanaomiliki shule kwa maana ya vijiji na wanainchi wao wapewe elimu juu ya uhitaji wa TEHAMA mashuleni.

Tatu Selikari ikubali kuwa sasa ni ulimwengu wa komputer na kuongeza mafungu yakuendeleza TEHAMA mashuleni.

TWENDE KAZINI.

MAPENDEKEZO YANGU JUU YA TEHAMA (INFORMATION TECHNOLOGY – (IT)) SHULENI NI HAYA

kila darasa liwe Kompyuta, power Point na Ubao wa kisasa(wenye asili ya kioo)

Ni vema kila mwanafunzi anatakiwa awe na kompyuta kwenye dawati/kiti chake lakini hatujafika huko KITEHAMA

Kompyuta :- Kutokana mwendokasi wa TEHEMA, mwalimu anatakiwa kutumia Kompyuta anapofundisha ili waweze kutoa maada zinazofanana kwa wakati mmoja nakupunguza kazi za karatasi (paper work) pia kuborasha utunzaji wa kumbukumbu za maada zilizofundishwa.

Power point:- Kufundisha kwa kusimulia kumepitwa na wakati, nadiyo maana watoto wanashika ya mitaani zaidi kwa sababu yanaonesha uhalisia, Mwanafunzi anapoona kitu halisi anavutiwa na udadisi kuwa mwalimu ametamka, ameona kwenye power point nawakati mwingine kaoneshwa picha za video mfano somo la baolojia akaiona chembe hai ilivyo hatasahau wala kupoteza kumbukumbu. akifundishwa madhara ya UKIMWI (VVU) akaoneshwa vedeo watu wanaoumwa, akaona kirusi kinavyoingia mwilini na nini kinakwenda kufanya, atakuwa na uelewa wa kwenda nao mitaani kupinga nadharia zilizozagaa zenye kuhamasisha mazingira ya aina hiyo, Mwanafunzi akijifunza namna ya kupanda miti ya matunda akaona vedeo zake, akirudi nyumbani atanzisha bustani yake kujibu kile alichojifunza na kuwa mwanzo wa kuwa na viwanda mbalimbali.

Ubao wa kisasa (usiotumia chaki):– Ubao huu utatumiwa na mwalimu kuelezea zaidi inapobidi hasa masomo ya sayansi na hesabu kupanua uelewa kwa mwanafunzi.

Mifano michahe hiyo inaweza kumuwezesha mwanafunzi kwenda kutengeneza ajira badara ya kusubiri na kupoteza fursa. siyo vibaya kama maamuzi.

Zinaweza kuteuliwa shule hata mbili tu kimkoa zikafanya majaribio kama hayo ya TEHAMA DARASA na baadaye tathimini ikafanyika kama kuna mafanikio au hapana.

Nashauri wadau wa elimu tuangazie MWENDOKASI WA TEHEMA NA NAMNA YA KUFUKUZIA HIYO KASI YAKE.

Tutarizika na mkoa wetu kama tutatumia mfano wa picha ya pili hapo juu lakini kama ni hiyo ya kwanza hatuwezi kufika kilahisi safari yetu.Nmaanisha matumizi a kili na teknologia ya kisasa,

UTALIPENDA TANGAZO HILI

SONGWE NI SALAMA UNANAJUA NI KWANINI? FUATILIA

1 SISI WOTE, TUMEPIMA MAAMBUKIZI YA VVU.

2 SISI WENYE VVU TUMEUNGANISHWA NA VITUO VYA HUDUMA KWA UANGALIZI NA MATIBABU,

3 SISI AMBAO HATUNA MAAMBUKIZI YA VVU, TUNACHUKUA HATUA SAHIHI KUJILINDA NA MAAMBUKIZI YA VVU

4 KIZURI ZAIDI SWALA LA MAENDELEO LINATUHUSU WOTE NI JUKUMU LA PAMOJA.

NI VIZURI NA WEWE UKASHAURI KWENU MFANYE HIVYOHIVYO KUIWEKA JAMII YENU SALAMA! UPO!!

Gabriel Gavu
BIASHARA MKOANI SONGWE.
Mtazamo wangu Magulio maarufu minada ifutwe kwasababu inaua biashara za kudumu.
1- minada inazuia mzunguko wa fedha wa kila siku kwa kuwapangia watu siku maalum za kununua/kutumi fedha zao
2- Inatoa fedha nyingi nje ya mkoa kwenda mikoa mama ambazo zingesaidia kuinua uchumi wa mikoa mipya Songwe inanyonywa na Mbeya kiuchumi kupitia minada.
3- Maduka mengi hayapanuki kwasababu ya uwepo wa minada. Chunguzeni vijiji vyote vyenye magulio maduka yao hayaongezeki mitaji na kwa maana hiyo huwezi kuwa na walipa kodi wazuri sababu biashara zao huathiriwa na gulio. Labda kwa upande wa mazao huenda kukawa na faida za uwepo wa magulio kiuchumi.

5 – Minada bidhaa nyingi hazilipiwi kodi popote na kuwapa mzigo wachache kuubeba mkoa husika kukidhi mafanikio ya malengo ya kukusanya kodi kimkoa.
Nashauri minada ifutwe kuokoa biashara zetu na kujiridhisha na hilo mdaharo uandaliwe kwa wafanyabiashara wenu msikie maoni yao juu ya hili. Asante.

Gabriel Gavu

SONGWE NINAYOITAKA MKOA WA SONGWE KUWA KIJANI YENYE TIJA INAWEZEKANA: – Kuugeuza Mkoa wa Songwe uwe wa kijani yenye tija inawezekana tukichukua hatua, Miji na vijiji vinatakiwa kupambwa kwa miti ya matunda SHIDA ni Ufugaji usio na tija wa mifugo michache yenye kuharibu mazingira. KUMBUKA WATU WANAONGEZEKA LAKINI MIPAKA HAIPANUKI.

1 Kuishawishi jamii ya Mkoa wa Songwe ichukie jangwa kwa kupanda miti ya matunda au mazao ya muda mrefu kuzunguka nyumba zao kama vile Miembe, Mikaranga, (karanga miti) Parachichi na mengine inaweza kuleta kijani yenye tija na ya pekee kwenye kuinua uchumi wa wakazi mkoani Songwe.

ukiamua kuchukua hatua basi nunua au andaa bustani ya matunda kwa kufuata ushauli wa wataalam wa kilimo. Upandaji miche huazia kwenye maandalizi ya mbegu, kituru na namna ya kupanda. tazama mfano wa upandaji usio na kiwango kwa mche wa mparachichi (avocado tree)

huu ni mparachichi uliogeuwa 1 sehemu ya mzizi mkuu ililekezwa juu hiyo ukiwa shambani baada ya kutoa eneo ulipopandwa mwanzo (kwenye bustani) kwa asilimia zaidi ya 80% utakauka. 2 viliba vyenye uwazi chini yaani havijafungwa au kushona kwenye upangaji wa mbegu za parachichi ni shida nyingine pia.
Mche wa mparachichi uliopandwa vizuri ukipelekwa shambani unaonesha maendeleo mazuri.

2 Watoto wa wakulima wfundishwe au wasome kilimo biashara il kuondokana na kilimo cha mazoea, sambamba na elimu kwa wazazi kutumbua kuwa kilimo ni ajira tosha kwa taifa letu.

3 Ufugaji uliopo usiyo na tija utokomezwe kwa kunusuru kijani na hasa Mbuzi wakati wa kiangazi ambapo kila mwenye mbuzi huwaachia huru. Jambo la kufanya a) -Watu wafuge kwa mifumo za zizi (zero grazing) mifugo isitoke b) Kama mfugaji anataka kufuga kwa kuchunga atuoneshe eneo alilolitenga yeye kwa ajiri ya mifugo yake. tofauti na sasa ambapo miti midogo inayoota kifuku, kiangazi inaharibiwa na mifugo mpaka migomba inaathiriwa na mnyama mharibifu zaidi na Mbuzi ni adui wa miti na matunda kwa maeneo yetu.

4 Kama njia hizo haziwezekani basi mtu huyo awe amepoteza sifa za kufuga. Haya yote yanaweza kusaidia kuinua upatikanaji wa kijani yenye tija kwa kilimo cha matunda mbalimbali na kuongeza kasi ya ukijani kuzunguka makazi ya jamii na kuondoa dhana ya kusema hujaenda sokoni hujala tunda. Ukipita maeneo mengi kwa sasa hakuna miti ya Matunda, Miti ya kupandwa midogo inayokuwa kwa sababu tu ikifika kiangazi kila mtu anaachia Mbuzi wake. Mfano mdogo tu, Rungwe Miparachichi na Ndizi inapendwa sana na Ngombe na Mbuzi lakini kwasababu hii mifugo haiachiwi ikazulula, popote migomba na miparachichi inapandwa na inakua. Sisi nini kinashindikana? Tujitabue haya yatawezekana.

JINA LA MBOZI NA HISTORIA YAKE

KAHAWA ni moja ya mazao yaliyoitangaza wilaya ya MBOZI kwa nguvu kubwa

Nimekuwa nikisoma kwenye mitandao kuwa jina Mbozi lilitokana na neno Mbozyo hivyo ujio wa wageni walishindwa kutamka Mbozyo na kusema Mbozi, Mimi bado siriziki sana na kuwa ilikuwa hivyo. Ebu tutazame na hili.

Kuna Habari kuwa kulikuwa na mtu jina lake Mwambozi aliishi maeneo ambayo leo hii panaitwa Mbozi Mission. hili jina huenda ndiyo chanzo sahihi cha jina Mbozi. kwa nyongeza zaidi huyo mtu alihama baadaye na kuhamia eneo moja Mgamba nafuko, sehemu hiyo pia ilikuja kujulikana kama Mbozi namba 2. tunaweza kuwatafuta wazee wa maeneo hayo kupata maarifa ya kihisoria zaidi kuhusu Jina hilo. ni katika kujifunza, tuongezeane utaalaam zaidi. Toa mawazo yako.

MALUMBANO YA HOJA yasiyo ya KISIASA ni jambo linaloweza kuendeleza Mkoa wa songwe. kwa kuwa tuna vyombo vya habari inaweza kutengwa siku moja kila mwezi watu wapewe nafasi waongee, wasikilize, watoe maoni yao na changamoto wanazozipata,. Viongozi waandamizi wanaweza kupata kitu kutoka kwa wadau wa midahalo hiyo.

MALUMBANO YA HOJA NDIYO YENYE NAFASI HAPA ILI KUIJENGA SONGWE IMAYOPENDEZA. SIYO VIBAYA KUJADIRI HATA TANZANIA UNAITAKA. Naanza mimi. Napenda Mkoa wa Songwe uwe na Barabara ya pili kutoka Mahenje mpaka Tunduma kabla jiji la Songwe halijashona, ili kuepusha adha ya bomoa bomoa inayowapata Dar-es-Salaam, Mbeya na Mwanza kupisha miundombinu ya Barabara. Lakini pia ni kulipamba jiji tarajiwa la Mkoa wa Songwe kwa miaka ya hivi karibuni. tutarajie vitu kama hivi.

Ndoto zinazoweza kutokea

MABASI YA MZUNGUKO (DALADALA) MKOA WA SONGWE. Napendekeza kuwe na mfumo wa babasi ya mzunguko kutoka Mulowo mpaka Tunduma, Biashara hiyo itolewe na kampuni kwa mfumo kama wa mabasi ya mwendokasi Dar. Wenye mabasi hayo yawe madogo au makubwa wasiruhusiwe kujiendesha bali wakabidhi kwenye kampuni itakayo kuwa ina kibali hicho kuendesha biashara hiyo, mwenye basi alipwe kwa mwezi. Hii itasababisha yafuatayo:-

1Madeleva wataajiriwa kwa mikataba inayofuata haki za kitumishi na watapata mafunzo ya utunzaji wa magari, kulinda ajira na kuiheshimu kazi yao, kuheshimu na kutii alama za barabarani, na kuleta usafiri wenye mfumo unaovutia wageni na kulipa jiji La Songwe tarajiwa hadhi ya pekee.http://ihoma.org

2Kutakuwa na huduma isiyo na msongamano wa kushindana kwa kwa kuwa magari yote yatakuwa yanafanya kazi ya kampuni moja.

3kutakuwa na fursa ya kukodisha magari kwa wageni wa kitalii na kwa wenye kazi maalum bila usumbufu mfano wakati wa mitihani ya shule za msingi na wakati wa uchaguzi na matukio mengine maalum. Faida zingine changia mtazamo wako tukae kwenye jiji moja.

KIJUE KIMODO CHA MBOZI

Kimondo cha Mbozi hakijulikani kilikuja lini duniani

Kupiga picha kwenye kimondo cha Mbozi ni tukio la kipekee kwenye kivutio cha utalii kilichopo wilayani Mbozi, mkoa wa Songwe, Nyanda za Juu Kusini nchini Tanzania.

“Wengi huwa wanafurahia kupiga picha kwa sababu ni kitu cha kipekee na tunaamini kuwa mtu akishapiga picha anakuwa balozi wa kimondo hiki kwa wengine,” anasimulia Beatus Bonabana, Mhifadhi, kivutio cha Kimondo Mbozi, anaongeza akisema. Katika miaka ya nyuma, wenyeji wa eneo hilo walikuwa wanatumia sehemu hiyo kwa ajili ya maombi ya kupata kitu, walifanya matambiko, ni jambo linaloendelea kufanyika mpaka leo. “Kimondo cha Mbozi kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 12 na ni cha nane kwa ukubwa duniani. Ni cha pili Afrika baada ya kimondo cha Hoba chenye tani 60. Kimondo cha Hoba kilichopo nchini Namibia ndicho kikubwa zaidi Afrika na duniani. Haijulikani ni lini hasa kimondo hiki cha Mbozi kilianguka, ila mtu wa kwanza kukiona katika miaka ya 1930 alijulikana kwa jina la Halele Simbaya, ambaye alikuwa mhunzi. Halele alipogundua kimondo hiki alitoa taarifa kijijini kwao, ndipo wenyeji wakaanza kuabudu katika shimo ambalo huwa linahifadhi maji ambayo wenyeji hunawa kupata baraka na wakaliita tukio hilo kuwa ni kusafisha nyota. Zamani kimondo hiki kilikuwa kinang’aa lakini sasa kimekuwa na rangi nyeusi baada ya kuathiriwa na hali ya hewa. Kimondo hiki hakifanani na chuma aina nyingine kutokana na ugumu wake na ukikipiga ni kama kuna uwazi ndani yake, unasikika mlio wa sauti ambao ni tofauti.

Sauti inayoonesha kuwa ndani kuna uwazi na hii inatokana na madini ambayo yaliyokiumba.

Imani kuhusu kimondo haipo miongoni mwa wenyeji hao wa Mbozi tu, bali sehemu mbali mbali duniani ambako vinapatikana.

Wenyeji wake huhusisha zaidi na nguvu za Kimungu, hivyo kuyafanya maeneo vilipoangukia kuwa maeneo matakatifu kwa misingi ya imani zao.

Mambo matatu kukihusu kimondo cha Mbozi

  • Kimondo cha Mbozi kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 12
  • Ni cha nane kwa ukubwa duniani
  • Cha pili Afrika baada ya kimondo cha Hoba chenye tani 60.
  • Inaaminika mtu wa kwanza kukiona katika miaka ya 1930 ni Halele Simbaya.
  • Hakipati joto la jua kali hata katika msimu wa kiangazi.

Inaelezwa kuwa tangu zama za kale, vimondo viliaminika kuwa vitu vitakatifu na jamii mbali mbali za wakati huo duniani. Utaratibu wake wa kuanguka hapa duniani, ambapo huambatana na mwanga na sauti, kama vile nyota idondokayo, vumbi na kishindo imekuwa siku zote ikisababisha hofu kwa wale walioshuhudia. Kimondo hiki huwa ni baridi wakati wote, hata wakati wa msimu wa kiangazi ambapo jua huwa kali sana, lakini bado huwa cha baridi. Hiki ni kimondo kikongwe duniani kwa sababu hata hakijajulikana kilianza kuwepo hapo tangu lini tofauti na vimondo vingine duniani vinajulikana vilianguka lini (tarehe au mwaka) au kuonekana athari zilizosababishwa na kuanguka kwa kimondo hicho. Mfano kimondo kikianguka na kugongana na uso wa ardhi huwa kinaharibu makaazi ya watu au kama ni msituni miti pia huvunjika na kina tabia ya kujichimbia. Mfano kimondo kikubwa duniani ambacho kipo Namibia, kilipogonga uso wa ardhi kilijifukia.

Moja ya vivutio Wilaya ya Momba ni pamoja na Bwawa la Chumvi. Bwawa hili chumvi inayofaa kwa matumizi ya binadamu huvunwa hapa. ni chumvi ambayo inahitaji tu kuiongeza madini ya chuma (IODINE) na mzingira ya usafi katika taratibu zake za uvunaji. Fika mwenyewe ufurahisha nafsi yako.

Bwawa la chumvi – Itumbula, Kata ya Ivuna wilayani Momba

UJENZI WA BWAWA WA CHUMVI KATIKA KATA YA IVUNA -ITUMBULA

Hatua mbalimbali zinazochukuliwa kuliboresha Bwawa la chumvi

VIVUTIO

KIMONDO

One Reply to “MKOA WA SONGWE NINAOUTAKA”

Leave a Reply